Tiririka

de Yammi

Mhh mhh
Ahh

Mapenzi yamenibadilisha
Siku hizi sinaga ubabe
Nishakuwa gucha
Niache moyoni niyabebe babe
Mimi ni kuku wako
Ukitaka mayai niyatage sema
Na ukiona na ujinga
We nisitiri usinibwage
Sina matamanio nishavukaga uko
Sinto ivua vazi la heshima
Ulionivisha kwa upendo
Sina matarajio
Yakuondoka kwako
Dunia imeshabadili wengi
Wakawa vituko

Mapenzi sio mchezo wa ngumi
Nipige na khanga au ukuni
Hata ukinifinya finya haiumi
Naona raha
Naisoma namba kwa kirumi
Huu mchezo gani mbona wakihuni
Hata ukinifinya finya haiumi
Aah naona raha
Unanijaza upendo mpaka unatiririka

Tiriririi
Unanitiririka Tiriririi
Tiriririi Tiriririi
Upendo unanitiririka mie
Tiriririi Tiriririi
Ahaa ahaa

Tiriririka kama si diaba
Najaza ndoo
Raha nazompa
Eti kama marhaba
Nikimpa shikamoo
Haniachi njiani nafika
Mi kwake Yes sisemi No
Siwezagi kususa
Nisipomuona wafukuta moyo
Asante angalau
Umenionesha maana ya upendo
Na sio kwa nahau (kwa nahau)
Umenionesha kwa vitendo
Sitokaaga nisahau
Nilinyanyasika hapo mwanzo
Niliyaoga madharau
Kwa kumpenda asiojali upendo

Mapenzi sio mchezo wa ngumi
Nipige na khanga au ukuni
Hata ukinifinya finya haiumi
Naona raha
Naisoma namba kwa kirumi
Huu mchezo gani mbona wakihuni
Hata ukinifinya finya haiumi
Aah naona raha
Unanijaza upendo mpaka unatiririka

Tiriririi
Unanitiririka Tiriririi
Tiriririi Tiriririi
Upendo unanitiririka mie
Tiriririi Tiriririi

Más canciones de Yammi