Inna di Club

de ISHA

Bure mwapapatika maasidi, na wazushi niye
Izo zenu heka heka mimi hazinikondeshi mie
Majungu mnayopika yanapita kama moshi mie
Mimi nimekamilika Kwangu mie hamnitoshi nyie
Naringia fungu langu alilonipa maanani mie
Kama mwaona uchungu pandeni ngazi mkazibe nyiee

Wanikera bure wanikera bure
Namie sio levo yako nasemaa
Oyaya ayee
Wanikera bure wanikera bure
Namie sio levo yako nasemaa
Oyaya ayee

Ati Nileweeh nipeni pombe nilewee nileewee
Kisha nifunge Mkaja nikaucheze msewee
Asidi wa rolo yangu ninamjua mwenyewee
Nilewee nipeni pombe nilewee
Kisha nifunge Mkaja nikaucheze msewee
Asidi wa rolo yangu ninamjua mwenyewee
Asidi wa rolo yangu ninamjua mwenyewee

Mimi yote nafaham nyie kila mliokusudia
Mwafanya juu chini mambo mimi kuniharibia
Mimi kufanikiwa wazi roho zenu zaumia
Nyie wapishi wa sumu pikeni nami nakuja chochea
Amenifanya tofauti vikuto vyenu sita umia

Wanikera bure wanikera bure
Namie sio levo yako nasemaa
Oyaya ayee
Wanikera bure wanikera bure
Namie sio levo yako nasemaa
Oyaya ayee

Ati Nileweeeh nipeni pombe nileweee nileewee
Kisha nifunge Mkaja nikaucheze msewee
Asidi wa rolo yangu ninamjua mwenyewee
Nilewee nipeni pombe nilewee
Kisha nifunge Mkaja nikaucheze msewee
Asidi wa rolo yangu ninamjua mwenyewee
Asidi wa rolo yangu ninamjua mwenyewee

Wanita midomoni nilicho wakosea mi nini
Kutwa kucha vikaoni naminaomba nijulisheni
Mbio zenu za sakafuni zitaishia ukingoni
Alienipa manani wakunizuia nani

Si levo yako (mimi)
Si levo yako (ooh mimi)
Si levo yako (mimi)
Si levo yako

Más canciones de ISHA