2K5 (Katana Riddim)

de ISHA

Wahenga walisema
Penzi lamea penye penzi
Twendelee kupendana
Japo wapo wanaoumia

Sasa naiona
Sasa naiona dhamani ya mapenzi
Kwako mimi
Kwako nimedidimia

Vile tu tulienzi
Hata kwa ugali na bamia
Tubembelezane kwa tamu tenzi
Hata tunapoikosa mia

Vimba mpenzi (vimba)
Jidai mpenzi (vimba)
Aah tamba mpenzi
Vimbaa, vimba

Vimba mpenzi wangu eeh (vimba)
Jidai beiby wangu eeh (vimba)
Aah tamba mpenzi wangu eeh
Vimbaa, vimba

Pua pua wanaokejeli
Chaguo langu mama mama
Ukitazama kuwaliko wao ni vituko

Furaha
Furaha imetambaa kwangu
Wao kila siku
Msukosuko

Wanajijaza masusu
Na mambo yasowahusu
Tusipuuze zao figisu
Vikwazo tusiruhusu

Vimba mpenzi (vimba)
Jidai mpenzi (vimba)
Aah tamba mpenzi
Vimbaa, vimba

Vimba mpenzi wangu eeh (vimba)
Jidai beiby wangu eeh (vimba)
Aah tamba mpenzi wangu eeh
Vimbaa, vimba

Tupendane kwa hali na mali mama
Tusiwe kama manenge na mandawa
Eeeh maadui wapambane na zao hali
Sie malavidavi, malavidavi mama aah

Ah subira huleta kilicho mbali
Kipendacho moyo ni dawa

Eeh mwaiona eeh (mwaiona)
Bendera yetu yapepea (mwaiona)
Safari yetu yaendelea (mwaiona)
Chuki zao twazipotezea (mwaiona)

Vimba mpenzi (vimba)
Jidai mpenzi (vimba)
Aah tamba mpenzi
Vimbaa, vimba

Vimba mpenzi wangu eeh (vimba)
Jidai beiby wangu eeh (vimba)
Aah tamba mpenzi wangu eeh
Vimbaa, vimba

Más canciones de ISHA